Tuesday 30 March 2010

ELIMU NA MAENDELEO

                                          Mheshimiwa James Mbatia


AFAFANUA MIFUMO YA ELIMU   ILIYO RASMI NA ISIYO RASMI TANZANIA

Mafanikio yote ya Sayansi na Teknolojia yametokana na mifumo ya elimu inayojali kwa kiasi kikubwa haki za binadamu na hasa uhuru wa kutoa mawazo na haki ya kushirikiana kimawazo.
Mataifa yote ambayo leo yanafanya vizuri katika uwanja wa kiteknolojia, yamefikia kiwango hicho baada ya kutilia maanani umuhimu wa kuzingatia haki za binadamu katika kuendesha mifumo yao ya elimu ili kuweza kupambana na adui ujinga.

Hapa kwetu Tanzania tangu tulipopata uhuru , zaidi ya miongo minnne sasa tumekuwa tukisema tunapambana na maadui watatu : ujinga, maradhi na umaskini.
Hivi sasa kuna mwelekeo katika jamii yetu kurasmisha "rushwa' kuwa adui wa nne. Adui ni adui na sifa yake kubwa ni kujificha na kujitunza katika giza liloko katika jamii, giza la kutokuelewa, giza la kutojijengea maarifa  na ujuzi wa kuendana na mabadiliko ya dunia.
Maradhi, umaskini na rushwa ni maadui wanaosimamiwa na kuongozwa na adui ujinga.Ujinga ni hali ya mwanadamu kutotambua thamani yake, na yuko hapa duniani kwa sabau gani.
Jamii mbalimbali zinanjia tofauti ya kufafanua nini maana ya kuwa binadamu, utu ni kitu gani; binadamu anajitambua vipi kwamba ana utu; na je jamii yenye utu inafananaje? yote haya yanapaswa kufafanuliwa kufuatia mfumo wa elimu ya jamii.
Mfumo wa elimu ni jumla ya njia zote zinazotumika  na mwanadamu, katika kupata habri a taarifa katika mazingira aliyomo, kwa ajili ya maendeleo yake binafsi na maeneleo ya jamii yake kwa ujumla. Msamiati unaotumika  leo kimataifa, tunasema mifumo ya elimu ni kwa ajili ya kuleta maendeleo endelevu katika jamii.

Kuna mfumo miwili au mitatu ya elimu, mfumo mmoja unaitwa 'mfumo rasmi' na mfumo wapili 'mfumo usio rasmi' . Mfumo wetu rasmi ni ule unaosimamiwa na wizara ya elimu. Watanzania tumekua makini zaidi katika mfumo ulio rasmi kuliko mifumo isiyo rasmi.
Katika safari yetu ipitayo katika giza la ujinga , tumejikuta tumekwisha kujenga mfumo rasmi wa elimu ambao unavunja haki za binadamu.
Kuna dhana isiyo sahihi katika taifa letu ya kutambua mfumo rasmi wa elimu ni ule unaoambatana na mbwembwe nyingi za kuwepo kwenye majengi mazuri  yenye vyumba vizuri vya madarasa, madawati na samani nyinginezo kwa kikundi kidogo tu cha wananchi.

Mtazamo wa namna hio ni finyu, kwani unasahau kwani unasahau elimu iliyojali utu  inatokana  na mchakato mpana zaidi hasa kwa mawasiliano  kati ya mwalimu mwenye vitendea kazi bora vya kufundishia na ujuzi wakufundisha , na mwanafunzi mwenye utayari wa kujifunza.
Mifumo ya elimu yenye kujali utu, itatuwezesha kujenga taifa lenye uwezo wa kubuni mbinu zakukabiliana na mazingira yetu badala ya kutumia mawazo kutoka sehemu nyingine duniani hasa kutoka katika mataifa yanayoitwa 'yameendelea'.

Yatupasa  sasa kujenga dhamira ya kijamii ya kukubali kwamba elimu yenye kujali utu ndio mipango ya moyo ya Taifa letu.elimu isiyojali utu haina thamani kwa taifa letu.

Jacksom Makweta (Mb) alipokuwa waziri wetu wa sayansi na , teknolojia na elimu ya juu, kwenye kipindi cha kwanza cha serikali ya awamu yatatu alipenda sana kutuasa watanzania mara kwa mara kwa kusema naomba kunukuu "ukitaka kuua taifa lolote duniani, anza kwa kuua mfumo wa elimu"

Naomba nirudie kwa kusema kwamba kiongozi mkuu wa maadui wa taifa letu ni adui ujinga.Safari a kwenye giza hukumbwa na ajali nyingi, huambatana na kupoteza mwelekeo.Nguvu a dhoruba inayotikisa taifa letu kwa sasa inatokana na mifumo ya elimu isiyojali utu.

Tunaweza kupiga hatua za haraja haraka katika safari yetu ya maendeleo , hususani katika karne hii ya sayansi na teknolojia kwa kukubali kwamba , katika taifa letu tunahitajimtazamo mpya na mpana zaidi kwa mifumo yetu ya elimu.

Hatuna budi kama taifa kukubaliana na ukweli kwamba, ni wajibu na haki yetu sote kushiriki pamoja katika majadiliano ya kina na hatimaye tukubaliane kujenga mifumo ya elimu amabyo itawaandaa kimaarifa  Mtaanzania wa leo na kesho, mifumo isiyokua  na ubaguzi wa kimatabaka, kidini na au kikabila.Hii itatusaidia kuw ana taifa lenye uelewa unaofanana kimaadili na kiutamaduni.

No comments:

Post a Comment